HATI YA HUDUMA KWA WANANCHI
| NAMBA |
HUDUMA |
MAHITAJI (WAJIBU WA MTEJA) | MUDA WA UTEKELEZAJI |
| 1. | Matangazo ya nafasi za ajira | Tuma maombi katika ofisi za Bodi ya Utumishi wa Umma. | Maombi ya uajiri yanatakiwa kuwasilishwa ndani ya siku 21 kuanzia tarehe ya tangazo |
| 2. | Kualika walioteuliwa kwa usaili | Kujiandaa kwa usaili | Ndani ya miezi 2 baada ya tarehe ya mwisho ya kutuma maombi. |
| 3. | Kufanya usaili kwa walioteuliwa | Kuhudhuria usaili na kuwasilisha vitambulisho halisi, vyeti vya kitaaluma na kitaalamu. | Vyeti viwasilishwe wakati wa usaili. |
| 4. | Kutolewa kwa barua za ajira kwa waliofaulu | Aliyefaulu, kuwasilisha nakala halisi na zilizoidhinishwa za kitambulisho, vyeti vya kitaaluma, kitaalamu na vyeti vya utiifu wa kisheria kulingana na sura ya sita (6) ya Katiba ya Kenya, 2010. | Muda usiozidi mwezi mmoja (1) kuanzia tarehe ya mwito wa barua ya kazi. |
| 5. | Kuwashirikisha wanafunzi kwa mafunzo ya vitendo | Mwanafunzi awasilishe nakala zifuatazo kwa ofisi ya Bodi ya utumishi wa umma:
|
Majibu kutolewa ndani ya siku kumi na nne (14) kuanzia tarehe ya kuwasilisha ombi. |
| 6. | Kushughulikia Malalamishi/rufaa | Malalamishi/rufaa rasmi yawasilishwe kwa Afisa Mkuu Mtendaji/Katibu wa Bodi kupitia S.L.P 491-80108 Kilifi au Barua pepe: |
Malalamishi kushuhulikiwa na kutoa urejesho kwa mda usio usiopungua siku thalathini (30) |
| 7. | Kufuatilia na kutekeleza Kanuni za Maadili na Mwenendo kwa maafisa wa umma | Kujifahamisha na Kanuni za Maadili ya utumishi wa umma na kuripoti visa vya kutofuata kanuni hizo kwa Bodi ya utumishi wa umma. | Inaendelea |
| 8. | Kusuluhisha mashauri ya kinidhamu na rufaa katika Utumishi wa Umma | Uwasilishaji wa mapendekezo kutoka kwa afisi ya mkuu wa utumishi wa umma katika serikali ya kaunti. | Miezi sita (6) kuanzia tarehe ya kuwasilisha kesi kwa Bodi. |
| 9. | Huduma za mapokezi/kuhudumia wageni katika ofisi za Bodi wenye au wasio na miadi | Zingatia heshima, uwazi na mpangilio katika maombi yako. | Kwa muda usiozidi dakika kumi (10) |
| 10. | Kujibu simu | Kutoa maelezo wazi na mahsusi na kutumia nambari sahihi ya simu. | Muda usiozidi dakika tano (5) |
| 11. | Kusimamia fomu za maelezo ya mali na madeni katika utumishi wa umma |
|
|
| 12. | Kuidhinisha programu za mafunzo na maendeleo ya wafanyakazi zinazochukua muda wa zaidi ya miezi sita (6) | Uwasilishaji wa mapendekezo kutoka kwa afisi ya mkuu wa utumishi wa umma katika serikali ya kaunti. | Ndani ya mwezi 1 baada ya kupokea mapendekezo. |
| 13. | Kupandishwa cheo, Usaili wa ufaafu, Mabadiliko ya kazi, Uthibitisho wa ajira kwa maafisa | Uwasilishaji wa mapendekezo kutoka kwa afisi ya mkuu wa utumishi wa umma katika serikali ya kaunti. | Ndani ya mwezi 1 baada ya kupokea mapendekezo. |
| 14. | Kujibu barua na maswali ya jumla yaliyotumwa kwa Bodi kupitia barua pepe | Kutuma barua na maswali kwa Afisa Mkuu Mtendaji/Katibu wa Bodi, Bodi ya utumishi wa Umma ya Kaunti ya Kilifi, Kilifi Plaza, Ghorofa ya 2 au S.L.P 491-80108 Kilifi au |
Muda usiozidi siku kumi na nne (14) kuanzia tarehe ya kupokea. |
